Fahad Musana, ambaye ni shabiki wa
kutupwa wa klabu ya soka ya Chelsea, amefariki dunia baada ya mchezaji
wa zamani wa klabu hiyo, Frank lampard, kuifungia Manchester City bao la
kusawazisha, katika pambano lililopigwa jana baina ya timu hizo mbili.
Musana, mwenye umri wa miaka 24, na
ambaye alikuwa mcheza kandanda la kulipwa nchini Uganda, alikuwa
akitizama mechi hiyo iliyovuta hisia za mashabiki wengi katika kona
mbalimbali za dunia, na alianguka na kuzimia mara baada ya Lampard
kusawazisha bao, ikiwa ni dakika chache sana tangu aingie kutokea
benchi, katika dakika za lala salama.
Alithibitishwa kuwa amefariki baada ya
kuwasili katika hospitali ya
kijeshi ya Bombo, na rafiki wa karibu wa marehemu amenukuliwa na vyombo vya habari akisema “Jamaa, amekuwa ni shabiki wa kweli wa Chelsea, ambaye angeweza kufanya lolote lile kwa ajili ya klabu hiyo. Tulifanya naye mazoezi asubuhi ya jumapili, na hata mchana tukala chakula cha mchana pamoja, hakika inasikitisha”
kijeshi ya Bombo, na rafiki wa karibu wa marehemu amenukuliwa na vyombo vya habari akisema “Jamaa, amekuwa ni shabiki wa kweli wa Chelsea, ambaye angeweza kufanya lolote lile kwa ajili ya klabu hiyo. Tulifanya naye mazoezi asubuhi ya jumapili, na hata mchana tukala chakula cha mchana pamoja, hakika inasikitisha”
Tukio hili la kusikitisha,
limethibitishwa na Shirikisho la vyama vya soka nchini Uganda (FUFA),
ambalo limetoa tamko lake kufuatia mkasa huu wa kushtusha.
“FUFA, limekumbwa na mshtuko baada ya
kupokea taarifa za kifo cha ghafla cha mchezaji wa klabu ya Simba ya
Uganda, Misana Fahad, katika hospitali ya Bombo. Mwili wa marehemu bado
uko hospitalini hapo, na taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa
zitatolewa baadae”, sehemu ya taarifa ya FUFA imesomeka hivyo.
Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki wa
soka kufariki kufuatia timu wanazozishabikia kushindwa kuibuka na
ushindi katika mechi zao. Kumbukumbu za hivi karibuni sana kwa ukanda
wetu wa Afrika Mashariki na Kati, ni za shabiki mwingine wa soka
aliyefariki dunia msimu uliopita, baada ya timu aliyokuwa akiishabikia
ya Manchester United kupoteza moja ya mapambano yake, ilipokuwa chini ya
kocha David Moyes
No comments:
Post a Comment