Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha
mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza kukuweka katika hali
ya kufa kupona.
Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi,
baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza
simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri
alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha
mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni
kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.
Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo
bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika
magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.
Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati
mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza
kimagendo.
No comments:
Post a Comment