Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo
amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko
Haram.
Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu
wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu
na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa.
Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu
wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo
katika jimbo hilo kufungwa.
Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini
mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu
No comments:
Post a Comment