Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na
mwandani wake Amama Mbabazi.
Kwenye taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa
mchango wake kwa nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana
Rugunda ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.
Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa
mpinzani wa
Museveni katika uchaguzi ujao.
Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan
Rugunda kama waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara
moja.
Mbabzi alikuwa mwandani wa karibu wa Rais Museveni.
Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa
angemrithi rais Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa
huo uhusiano kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.
Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio
kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28
atakuwa mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu
chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.
Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali
alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
No comments:
Post a Comment