Pages

Tuesday, September 23, 2014

MVUTANO MKALI WAIBUKA NDANI YA BUNGE LA KATIBA SOMA NA SIKILIZA HAPA


Mvutano mkali umeibuka miongoni mwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu mabadiliko ya kanuni yanayofanywa ili kuwaruhusu wajumbe wa Bunge hilo waliopo nje ya Bunge kwa sababu mbalimbali, kupata fursa ya kupiga kura kutoka ndani na nje ya nchi.

Miongoni kwa wajumbe waliopinga marekebisho hayo ni pamoja na EZEKIEL OLUOCH na SAID ARFI ambao wamebainisha kuwa ni kinyume cha sheria kumruhusu mtu ambaye yuko nje ya Bunge kupiga kura kutokana na umuhimu wa maamuzi yanayotarajiwa kutolewa, ambapo michango yao imekuwa ikikatizwa mara kwa mara na maombi ya kutoa taarifa.
Licha ya wajumbe hao kupinga marekebisho hayo ya kanuni za Bunge 



Maalum la Katiba, wajumbe wengi waliunga mkono mapendekezo hayo ambayo pia yanawezesha kupigwa  kura ndani ya muda uliopangwa wa siku sitini akiwemo PAUL MAKONDA na PINDI CHANA.
Katika mjadala huo miongozo mbalimbali imeombwa hasa kwa wajumbe waliokwenda kwenye Ibada ya Hijja hali iliyomuinua kitini mjumbe wa Bunge hilo Sheikhe THABIT JONGO na kutolea ufafanuzi jambo hilo baada ya kuomba muongozo wa mwenyekiti.
Mjadala huo ukahitimishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni PANDU AMEIR KIFICHO baada ya kupata wasaa wa kutolea ufafanuzi baadhi ya hoja na kuelezea muundo wa upigaji kura.
Kamati ya uandishi ya Bunge la Katiba inaendelea kuandaa Katiba inayopendekezwa kwa kuweka maoni mbalimbali yaliyotolewa na kamati 12 za Bunge hilo na kujadiliwa na Bunge zima ambapo Septemba 24 Katiba inayopendekezwa itawasilishwa bungeni na kupigiwa kura.

No comments:

Post a Comment