Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, September 11, 2014

MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS HAKUKUSUDIA KUUA MAHAKAMA YASEMA,HATMA YAKE NI KESHO

Mwanariadha Oscar Pistorius akilia wakati wa mapitio ya hukumu yake katika Mahakama Kuu jijini Pretoria.
JAJI anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.



Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda kosa alipomuua mpenzi wake Reeva.


Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi , akisema alidhani kuwa ni mwizi aliyekuwa amevamia nyumbani kwake.
Staa huyu huenda akafungwa jela miaka 25 kama atabainika kuua kwa kukusudia.
Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi, baada ya wapenzi hao kutofautiana. Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake kwa kukusudia. Oscar Pistorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao mwaka jana. Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake Reeva baaya ya ugomvi baina yao. Hukumu hiyo itaendelea kesho asubuhi.

No comments:

Post a Comment