Na Mwandishi wetu
POLISI
nchini Ujerumani wamefanikiwa kumkamata Promota mwenye asili ya nchi ya
Nigeria ambaye ndiye aliyesababisha fujo katika onyesho la msanii
Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ zilizotokea Agosti 30 mwaka huu
kwenye ukumbi wa Stuttgart nchini Ujerumani .
Kwa
mujibu wa chanzo cha habari kutoka nchini Ujerumani kilisema kwamba
Jeshi la Polisi nchini humo kilisema hadi kieleweke kwani watamchukulia
hatua kali ili iwe fundisho kwa mapromota kama huyo.
Jumamosi
iliyopita Awin Williams Akpomie (pichani) alisababisha fujo na kuvunjwa
kwa viti , vyombo vya muziki na vitu mbalimbali baada ya mashabiki
kushikwa na hasira kwa kukosa burudani ya shoo ya Diamond ambapo
alicheleweshwa na Promota huyo aliyewatangazia shoo kuanza kufanyika
saa nne usiku na badala yake kutaka shoo ifanyike saa kumi alfajiri.
Baada
ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji
wa onyesho hilo Akpomie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa
kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya African Party na mkutano sio onyesho
la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara kiasi
cha Euro 300,000 sawa na sh. Mil.600 za Kitanzania ambazo anatakiwa
azilipe.
Aidha
imeelezwa kwamba Akpomie hakuwa na bima ya kulinda onyesho hilo na
ukumbi lilipotarajiwa kufanyika onyesho hilo ambapo ni ukumbi wa
mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.
Taarifa
za kipolisi zinasema kwamba suala hilo tayari zimepeleka suala hilo
kwa ofisi ya Sheria ya mji wa Stuttgart zilikotokea fujo hizo ili
sheria ichukue mkondo wake.Hadi sasa bado Polisi wanaendelea kumhoji
Akpomie kutokana na tetesi kwamba najihusisha na biashara zingine za
haramu.
Wakati
huo huo Taasisi mbali mbali na jumuiya za Wafrika nchini Ujerumani na
jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa Nigeria Akpomiemie kwa
kuwadanganya mashabiki na kulivunjia hadhi sifa za bara la Afrika
nchini humo , pia taasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha
kabisa .
No comments:
Post a Comment