Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge –Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9 katika eneo la Lugalo, jijini Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar esalaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Muhandisi Musa Iyombe imeeleza kuwa sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zitafanyika tarehe 1, Oktoba ,2014 katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe kuanzia saa nne asubuhi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 12.9 ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
No comments:
Post a Comment