Pages

Saturday, September 27, 2014

SERENGETI SOKA BONANZA YAFANA NDANI YA JIJI LA MBEYA IKIWA NI AMSHA AMSHA YA FIESTA JUMAPILI TAR 28.09.2014

Wachezaji wa Timu ya Mpira ya Salalizya fc kutoka Mabatini wakiwa katika picha ya ukumbusho kabla ya mechi

Wachezaji wa timu ya baa ya Tugelepo ya Mbata wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi

Kikosi cha Timu ya Wanafunzi wa TIA wakiwa katika pozi

Wachezaji wa Timu ya Baa ya Kalembo ya Sokomatola wakisalimia wachezaji wenzao kabla ya kuanza mechi

Mshambuliaji hatari wa timu ya Tugelepo akiambaa na mpira katika mechi kali dhidi ya Salalizya ya Mabatini

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa Serengeti Fiesta 2014 katika viwanja vya TIA.

Mgeni rasmi wa Serengeti soccer Bonanza, Patrick Zambi ambaye ni mkurugenzi wa PADZ Hoteli akizungumza katika bonanza hilo

Baadhi ya watazamaji wakifuatilia kwa makini bonanza hilo

Mmoja wa Waandaaji wa Serengeti Fiesta 2014 Ibrahim Masoud akizungumza na mashabiki wa mpira wa miguu waliojitokeza kushuhudia Serengeti super bonanza




Mgeni rasmi akigawa zawadi kwa washindi







Mgeni rasmi Patrick Zambi akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Salalizya pamoja na zawadi zao baada ya kuibuka washindi wa kwanza.





TIMU ya Mpira wa Miguu kutoka Baa ya Salalizya iliyopo Mabatini jijini Mbeya imeibuka kidedea katika Bonanza lililoshirikisha Timu za Mabaa lililoandaliwa na Serengeti fiesta maarufu kwa jina la Serengeti Soccer Bonanza.

Katika Bonanza hilo lililozishirikisha Timu nne lilifanyika jana katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Mbeya(TIA) zikiwmo timu kutoka Baa ya Kalembo ya Sokomatola, Tugelepo ya Mbata na wenyeji Wanafunzi wa TIA.

Timu ya Salalizya fc ya Mabatini ilijinyakulia zawadi ya Katoni 8 za Bia aina ya Serengeti baada ya kuishinda timu ya Wanafunzi wa TIA katika fainali kwa magoli mawili kwa nunge hivyo TIA  kuibuka mshindi wa pili na kujinyakulia Katoni 4 za bia.

Awali timu ya Salalizya iliifunga Tugelepo goli moja kwa bila katika mchezo wa utangulizi na kasha timu ya TIA kuitoa timu ya Kalembo kwa mikwaju 9 kwa 8 baada ya muda wa kawaida kutofungana.

Mshindi wa tatu ilikuwa ni timu kutoka baa ya Kalembo baada ya kuifunga timu ya Tugelepo kwa mikwaju 4 kwa 2 ya penati katika kumtafuta mshindi wa tatu kutokana na kutoshana nguvu katika muda wa kawaida.

Hivyo Mshindi wa tatu alijipatia Katoni Mbili huku timu ya Tugeleo ikijipatia Katoni Moja kutokana na kuwa mshindi wa nne na wa mwisho.

Katika Bonanza hilo Mgeni rasmi aliyegawa zawadi kwa washindi alikuwa ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya PADZ iliyopo Forest Mpya, Patrick Zambi, ambaye alitoa wito kwa vijana kupenda michezo na kujikita katika mazoezi ili kuim,arisha afya zao.

Mwisho.

Na Mbeya yetu/Stanslaus Lambart

        



No comments:

Post a Comment