Pages

Friday, September 5, 2014

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI 8::MAJAMBAZI WATANO WAUAWA NA POLISI KIGOMA,



Majambazi watano waliokipata cha moto katika Majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakiwa na silaha za kivita wakisubiri kuteka magari Alfajiri ya Septemba 03,2014 wakiwa chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Kasulu.





 


JESHI la polisi mkoa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha za kivita aina ya SMG, mabomu matatu ya kutupa kwa mkono, risasi 64 pamoja na kuwauwa watu watano wanaosadiliwa kuwa ni majambazi wakati wa purukushani za majibizano baina majambazi hao na askari polisi mkoani Kigoma.Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo kamishina msaidizi wa polisi mkoa kamanda Japhal Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:45 alfajiri Septemba 3 mwaka huu, katika barabara kuu ya Kasulu – Kibondo eneo la pori la Malagalasi Wilayani Kasulu.Kwa mujibu wa kamanda Ibrahim alisema askari polisi wakiwa katika doria walipata taarifa za majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi wakitaka kufanya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha kuteka magari ya wasafiri yaliyokuwa yakipita katika barabara hiyo.Alisema kufuatia taarifa hiyo askari polisi walijipanga na kuweka mtego katika eneo lililokusudiwa kufanyika uhalifu huo ambapo baada ya muda watu hao walifika eneo la tukio ili kukamilisha azma yao ambapo askari waliwafuata ndipo walipoanza majibizano ya risasi na askari polisi.


Katika tukio hilo askari walifanikiwa kuwauwa majambazi wote watano ambapo katika eneo la tukio hilo walikuta mabomu matatu, silaha mbili za kivita aina ya SMG No. 691220 pamoja na AK 47 no. UA40501997 magazini tatu zenye risasi 64 sambamba na mikate na juice aina ya Zaam Zam orange kutoka katika kampuni ya Monas Beverages.


Kamanda alisema miili ya majambazi hao ipo katika hospitali ya wilaya ya Kasulu ambapo majina yao hayajatambulika huku askari polisi waliokuwa katika tukio hilo wakiwa wamesalimika na hakuna aliyejeruhiwa ambapo msako unaendelea katika maeneo yote ili kukomesha vitendo vya uhalifu mkoani Kigoma.

No comments:

Post a Comment