Pages

Wednesday, September 17, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE:::REAL MADRID WAITANDIKA BASLE GOLI 5 KWA 1

 Ligi ya mabingwa wa ulaya imeanza tena kwa michezo kadhaa kupigwa usiku wa leo huku mabingwa wa watetezi Real Madrid wakianza kuutetea ubingwa wao kwenye mchezo dhidi ya FC Basle.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Santiago


 Bernabeu umeisha kwa matokeo ya ushindi mzito kwa Real Madrid walioibamiza Basle 5-1.
Suchy alianza kujifunga goli kwenye dakika ya 14 na kuipa uongozi Madrid, kabla ya Gareth Bale kufungua ukurasa wake wa magoli kwenye UCL kwa kufunga goli la dakika ya 30, Cristiano Ronaldo akaongeza lingine dakika ya 31, James Rodriguez akafunga goli la 4 dakika ya 36, na Karim Benzema akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la FC Basle dakika ya 79.




No comments:

Post a Comment