Wanajeshi kumi na wawili nchini Nigeria wamepewa adhabu ya
kifo kwa uasi pamoja na jaribio la mauji.
Hii ni baada ya kumfyatuliwa bunduki afisa mkuu anayeongoza
operesheni ya kupambana dhidi ya kundi haramu la kiislamu la Boko Haram kati
mji wa Maiduguri,kaskazini Mashariki mwa nchi, mwezi wa Mei.
Wanajeshi wengine watano waliachiliwa baada ya ushahidi
kukosekana.
Wanajeshi hao 12 walipatikana na hatia ya kumfyatulia risasi
Jemedari amadu Mohammed.
Wanajeshi hao walikasirishwa na kamanda wao ambaye
walimlaumu kwa kukataa kuchukua hatua baada ya msafara wao kushambuliwa.
Jeshi la Nigeria limeshindwa kuwashinda Boko Haram na
wanajeshi wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokabiliana na wapiganaji wa Boko
Haram hawana silaha za kutosha kukabiliana nao.
Wote walikana mashtaka hayo katika Mahakama ya kijeshi mjini
Abuja.
Kitengo hicho cha Jeshi ndicho kinakabiliana na Boko Haram
Mahakama ya kijeshi ya watu tisa ilisikiza kuwa tukio hilo
lilitendeka baada ya kufyatuliwa kwa risasi kwa afisa mkuu wa kitengocha 7 cha
jeshi la Nigeria.
Ilimbidi Generali Amadu Mohammed kujificha walipomlenga na
bunduki zao.
Hata hivyo, hakuumia.
Kiongozi wa mahakama Chukwuemeka Okonkwoalisema kuwa hata
kama hukumu hizi zilikuwa chini ya udhibitisho wa mamlaka ya jeshi la Nigeria,
hakukuwa na shaka juu ya uzito wa kosa hilo.
Mwezi uliyopita, kundi la wanajeshi kaskazini masharikimwa
Nigeria walikataa kupambana na Boko Haram mpaka wapatiwe vifaa bora, mmoja wao
aliiambia BBC.
No comments:
Post a Comment