Mamia ya waandamanaj wa Hong Kong wamezingirwa na Askari
polisi wanaowataka kusitisha maandamano na mkusanyiko wao karibu na ofisi za
Makao makuu ya serikali.
Waratibu wa maandamano hayo wamekaidi amri hiyo na kuwataka
watu wengine zaidi kujitokeza ili kuwaunga mkono katika madai yao ya kuitaka
China iwaachie uhuru wa kumchagua kiongozi wao katika uchaguzi ujao wa mwaka
2017.
Kiongozi wa Mamlaka ya Hong Kong C Y Leung amesema serikali
yake imesikiliza na kuzingatia madai ya waandamani lakini inapingana na mpango
wao wa kujitenga.BBC
''Mimi na serikali yangu tutazingatia sheria za msingi na
uamuzi unaostahili wa NPCSC,tutajaribu juhudi zote kutekeleza uchaguzi wa
kiongozi mkuu kwa kila anayestahili kupiga kura atafanya hivyo mwaka 2017.
Serikali itaanzisha hatua inayofuata ya majadiliano kuboresha katiba hivi hivi
karibuni.
Inasihi sekta mbalimbali za jamii kushiriki katika
majadiliano yenye mantiki kwa Amani na kwa
kufuata sheria, kufikia makubaliano
na kukubali tofauti pamoja na kuruhusu watu milion tano wenye uhalali wa kupiga
kura hapa Hong Kong kumchagua kiongozi mkuu mwaka 2017 mtu mmoja kura moja''
amesema Leung Chung-ying.
'mimi na serikali yangu tumekuwa wasikivu kwa raia na
tumejitolea kudumisha jamii yote. Wananchi wanatakiwa kutoa wanayoyahitaji kwa
Amani, mantiki na kisheria, na kuheshimu na kuzingatia mitazamo mbalimbali
katika jamii.
Serikali ya SAR ya Hongkong imeazimia kupinga utawala usio
wa kisheria wa ofisi za serikali kuu au makao makuu ya wilaya 'utawala wa
seriakli kuu''. Polisi wanajitambua kukabiliana na hali kwa wakati
kwakuzingatia sheria'' Ameongeza
No comments:
Post a Comment