Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi kuanzia mwezi ujao, Oktoba 2014, itaanza zoezi la kuvihakiki
Vyama vya Kijamii hapa nchini.
Pamoja na mambo
mengine, zoezi hili linalenga kuvifuta kutoka katika daftari la Msajili vya
Vyama vya Kijamii vyama ambavyo vitabainika kuwa havina sifa tena ya kuendelea kuwa katika daftari hilo.
Vigezo ambavyo
vinaweza kusababisha chama kufutwa kutoka katika Daftari la Msajili wa Vyama
vya Kijamii ni pamoja na kutolipa ada za mwaka kwa wakati na kutowasilisha kwa
Msajili taarifa za kila mwaka
za utendaji kazi na mapato na matumizi ya fedha za chama husika. Kigezo kingine ni kwa chama kufanya shughuli tofauti na zile zilizoandikishwa katika katiba ya chama husika.
za utendaji kazi na mapato na matumizi ya fedha za chama husika. Kigezo kingine ni kwa chama kufanya shughuli tofauti na zile zilizoandikishwa katika katiba ya chama husika.
Ili kuvishirikisha
vyama husika, Wizara wakati wa kuanza zoezi hili itachapisha katika baadhi ya
magazeti majina ya vyama vyote vya kijamii vilivyopo katika kumbukumbu za
daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii.
Baada ya kutangaza
majina hayo, kila chama cha kijamii kitatakiwa kuhakikisha kuwa kimetekeleza
matakwa ya kisheria yaliyobainishwa wakati wa usajili wa chama husika.
Baada ya kipindi cha miezi mitatu tangu kutangazwa kwa
tangazo hilo, Wizara itaanza kuchukua hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na
kukifuta katika daftari la Msajili chama cha kijamii ambacho kitakuwa
hakijatekeleza matakwa hayo.
Aidha, pamoja na
mambo mengine, taarifa zitakazopatikana kutokana na zoezi hili la uhakiki pia
zitawezesha kuanzishwa kwa database
ya vyama vya kijamii ambayo
itasaidia kuboresha mawasiliano kati ya Msajili wa Vyama
na vyama hivyo.
Hadi sasa Daftari la
Msajili wa Vyama vya Kijamii linaonyesha kuwepo kwa vyama vya kijamii 9,554
kote nchini. Kati ya hivyo, vyama vya kidini ni 956 na vyama vingine 8,598.
Jukumu la kusajili na
kusimamia Vyama vya Kijamii linafanyika chini ya Sheria ya Vyama vya Kijamii
SURA 337 (Societies Act Cap. 337) iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
Vyama vinavyosajiliwa
chini ya Sheria hii ni pamoja na vyama vya kidini, vyama vya kitaaluma na vyama vya maendeleo ya kijamii.
Imetolewa na:
Isaac
J. Nantanga
MSEMAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment