Pages

Thursday, October 30, 2014

AJALI MBAYA YAUWA MWANAFUNZI PAPO HAPO MKOANI MARA

Mwanafunzi mmoja wa darasa la pili katika shule ya msingi Nyamikoma wilayani Butiama mkoani Mara amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na gari moja aina Toyota Prado yenye namba za usajili T767 dbx kasha kupaa na kuparamia nyumba na mashine ya unga katika eneo hilo la pida wilayani humo.

Ajali hiyo mbya imetokea katika eneo hilo la pida katika barabara kuu ya Mwanza-Sirari wakati gari hilo likitokea jijini Mwanza kwenda Nyamongo wilayani Tarime, ambapo imeelezwa kuwa baada ya kugongwa kwa mwanafunzi huyo Keneth Barnaba dereva wa gari alijitahidi kuwakwepa wanafunzi wengine lakini kutokana na mwendo 



kasi gari hilo lilimshinda na kupaa juu kisha kuvamia jengo la mashine ya kusagia nafaka na nyumba ya familia moja kijijini hapo.

Wakizungumza wakati wa maandalizi ya mazishi ya mwanafunzi huyo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, wameiomba wakala wa kuhudumia barabara nchini Tanroads mkoa wa Mara kuangalia uwezekano wa kuweka matuta katika eneo hilo ili kuzua ajali hizo za mara kwa mara.

Nao baadhi ya viongozi wa serikali katika kijiji hicho, wameitaka serikali kusikiliza kilio cha wananchi hao kwa madai kuwa katika kipindi kifupi tu tayari ajali kumi na moja zimetokea katika eneo hilo hatua ambayo sasa imefanya wanafunzi kuvuka barabara kupitia chini ya karavati hali ambayo imetajwa inaweza kuhatarisha maisha yao.

No comments:

Post a Comment