Mfanyakazi mmoja wa hoteli nchini Uingereza alilazimika
kutoa painti mbili za damu (Takriban lita moja) kutoka kwenye uume wake- baada
ya kusimama kwa muda wa saa 17 mfululizo.
Madaktari kwanza walijaribu kupunguza kasi ya damu kwa
kijana huyo, Jason Garnett, kwa kupiga sindano 24 moja kwa moka kwenye nyeti
zake.
Tovuti ya Metro imesema 'mashine' ilisimama kuanzia
siku ya
Ijumaa asubuhi alipoamka. Kijana huyo, 23, alijaribu kila aina ya njia, ikiwemo
kukimbia, na kuoga maji ya baridi sana, kabla ya kupelekwa hospitali na rafiki
yake.
Hospitali iligundua kuwa Garnett alikuwa na maradhi ambayo
ni haba kuonekana yajulikanayo kama priapism - ambapo uume husimama bila
kukoma. Maradhi hayo hayasababishwi na hamu ya kutaka kufanya mapenzi, lakini
iwapo mtu hatopata tiba, inaweza kuharibu uume, imeripoti tovuti ya
News.com.au.
Akizungumza na gazeti la The Sun, amesema: "Yaani
kuishia hospitali na jambo hili, ni moja ya siku ya aibu zaidi kwangu duniani.
"Kuona wakichoma sindano 'mashine' yangu ilikuwa jambo
gumu sana kwangu- kama kutazama filamu ya kutisha. Maumivu yalikuwa asilimia
100."
Amesema baada ya sakata hilo, nyeti yake ina majeraha
'kibao'.
Picha: © Getty Images / Peter Dazeley
No comments:
Post a Comment