Chama hicho cha National Congress Party kimesema kuwa jina
la Bashir pekee ndilo litakalowasilishwa kwa idhini ya chama hicho katika
kongamano litakalofanyika kuanzia Almisi.
Rais Bashir anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai
kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kivita katika jimbo la Darfur ambapo watu
300,000 wameuawa huku wengine milioni mbili wakitoroka kwao tangu waasi
walipoanza kupigana na serikali ya Bahsir mwaka 2003.
Amekanusha madai hayo huku Sudan ikikataa kuwa na ushikiano na mahakama ya ICC.
Bashir aliteuliwa kama kiongozi wa chama pamoja na mgombea mkuu wa chama hicho katika uchaguzi ujao.
Alishinda kuraa 266 kati ya kura 522 na viongozi wa chama wamesema watamwakilisha kwa kongamano la chama ili aweze kuidhinishwa.
Bashir mwenye umri wa miaka alichukua mamlaka kwa njia ya ,mapinduzina kuliwa na utata ikiwa ataghombea tena katika uchaguzi huo utakaofanyika mwezi Aprili.
uchaguzi huo utakuwa wa pili tangu mapinduzi yaliyopmuingiza mamlakani Bashir mwaka 1989.
No comments:
Post a Comment