Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, October 12, 2014

BINTI WA MH. MBUNGE ATWAA TAJI LA REDDS MISS TANZANIA,JIONEE PICHA 15 ILIVYOKUWA

Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam. Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.

Kwa ushindi huo, Sitti atapeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya Miss World 2015 na kajinyakulia kitita cha milioni 18 . 

Dorice Mollel ameshika nafasi ya nne wakati Nasreen Abdul akichukua nafasi ya tano.



 Pichani ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika shindano la Redds Miss Tanzania 2014 linaloendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar. Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tano bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya pichani kulia Ommy Dimpoz akitumbuiza jukwaani akiwa sambamba na msanii Vanessa Mdee mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),waliofika kushuhudia shindano hilo.Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 15 mara baada ya kuchujwa.  Sehemu ya baadahi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye shindano hilo la kumsaka Kinara wa Redds Miss Tanzania 2014 
Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakicheza moja ya onesho lao la ufunguzi wa shindano hilo,ambapo mshindi atatangazwa usiku huu na kujinyakulia kiasi cha shilingi miloni 18 taslim. Baadhi ya Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014,wakiwa jukwaani na mavazi ya ufukweni.  Msaniii wa Muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee a.k.a V-Money akitumbuiza kwenye shindano la kumsaka mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014,yanayofanyika usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa Mlimani,jijini Dar.  Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakikatiza jukwaani na mavazi yao ya ubunifu Baadhi ya Majaji wakifuatilia kwa makini Pichani ni Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 30 wakiwa jukwaani tayari kwa kuanza kuchujwa kupata washiriki 15 bora.

No comments:

Post a Comment