Pages

Friday, October 24, 2014

Boko Haram lawateka wanawake wengine

Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, zinasema kuwa idadi kubwa ya wanawake wengine wametekwa nyara na kundi la wapiganaji la Boko Haram.
Wiki jana maafisa wakuu wa nchi hiyo walitangaza kuafikia makubaliano ya kusitisha vita na kundi hilo.
Kwa hiyo kundi hilo lilikubali kuwaachilia wasichana zaidi ya miambli waliotekwa na kundi hilo kama 


sehemu ya makubaliano hayo miezi sita iliyopita.
Kulingana na taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, wapiganaji wa Boko Haram walishambulia vijiji viwili katika jimbo la Adamawa - Waga Mangoro na Garta.
Kisha wakawateka wasichana na wanawake wengi.
Vijini hivi vinapakana na miji ya Madagali na Michika ambayo imekuwa chini ya udhibiti wa wapiganaji hao kwa wiki kadhaa.

Kundi la kwanza la wasichana wlaiotekwa nyara na Boko Haram ambao bado kuachiliwa
Mashambulizi hayo yalifanyika Jumamosi siku moja tu baada ya jeshi la Nigeria kutangaza makubaliano ya kusitisha vita yameafikiwa na Boko Haram.
Kama sehemu ya makubaliano hayo, serikali ilisema wasichana 219 waliotekwa kutoka Chibok mwezi Aprili, wataachiliwa hivi karibuni.
Tangu tangazo hilo kutolewa, kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi, na hapajakuwa na kauli yoyote ikiwa wasichana wa Chibok wameachiliwa.
Kulingana na serikali, mazunguzmo yalitarajiwa kufanyika kati ya serikali na Boko Hara, wiki hii nchini Chad.
Wakati huohuo, polisi wanasema kuwa shambulizi lililofanywa katika jimbo la Bauchi liliwaua watu 5.

Licha ya kwamba mashambulizi yoyote yanayofanywa kaskazini mwa Nigeria hulaumiwa kwa Boko Haram, kundi hilo huwa kwa kawaida halijibu haraka na kwa hivyo huwa vigumu kuthibitisha kweli ikiwa ni wapiganaji hao waliofanya mashambulizi hayo.

No comments:

Post a Comment