Cristiano Ronaldo hana nia ya kurejea Manchester United na
atamalizia kucheza soka yake Real Madrid, amedai wakala wake Jorge Mandes.
Ronaldo, 29, tayari amefunga magoli 15 msimu huu, ikiwemo kufikisha hat trick
22 katika La Liga. Taarifa zimekuwa zikimhusisha Ronaldo kurejea Old Trafford
kwa uhamisho wa pauni milioni 80. Mendes amesema: "Cristiano ameridhika
sana Real Madrid. Ataendelea kuvunja rekodi zote hapo na kustaafu hapo."
Wakala huyo amekiambia kituo cha radio cha
Cadena COPE kuwa: "Huwezi
kupata mchezaji mwingine kama yeye.
"Anaendelea kuwa mchezaji bora, na ataendelea kuwa
hivyo hadi atakapofika umri wa miaka 40.
"Anaipenda United kwa sababu moyo wake ulikuwa pale kwa
miaka sita. Lakini sasa vyote anavyofikiria ni Real Madrid na atakuwepo hapo.
"Ndoto ya Cristiano ni kushinda Champions League. Huwa
bado ana njaa, na siku zote anataka zaidi.
"Haishi kushangaza watu. Ni vigumu kupata mtu yeyote
kama yeye katika historia ya soka."
Ronaldo aliondoka Manchester United kwenda Real Madrid mwaka
2009 kwa uhamisho wa pauni milioni 80.
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal alikiri mwezi
uliopita kuwa angependa kumsajili kiungo huyo, lakini hatarajii kama Real
Madrid watakuwa tayari kumuuza.
No comments:
Post a Comment