Mtandao wa kijamii wa Facebook umeahidi kujitahidi
kukabiliana na uuzaji na ununuzi wa 'Likes' bandia kwenye mtandao huo.
Facebook inasema imeshinda dola bilioni mbili katika kesi
iliyowasilisha mahakamani dhidi ya watu wanaouza 'Likes' za bandia kwa
wafanyabiashara walio na akaunti kwenye mtandao huo.
Inaarifiwa wamiliki wa makampuni wananunua 'Likes'
kwenye
mtandao huo ili akuanti zao kuonekana kuwa maarufu na kupendwa na watu wengine
wakati sio kweli.
Lakini Facebook imesema kuwa wanunuzi wa 'Likes' kwa njia za
kimagendo wanafanya jambo baya kwa wafanyabiashara wengine na ina maana kuwa
kampuni nyinginezo zenye akaunti zao kwa Facebook heunda zikapata hasara.
Katika taarifa yake, Facebook iliandika na kusema: 'Tunataka
kuhakikisha tunakomesha tabia ya ununuzi wa 'Likes' kwa sababu wenye biashara
na watu wa kawaida wanataka kuwasiliana kwa lengo la kupata mafanikio sio mambo
bandia. ''
Mtandao huo ulielezea kuwa wauzaji wa Likes bandia wanawapa
'admins' au wasimamizi wa akaunti fulani fursa ya kununua 'Likes' kama 10,000
bandia ili watu wapende akaunti zao.
Kwa sababu sakata kama hizi zinalenga zaidi kufaidika
kifedha na hasa kuwahadaa wafanyabiashara , tunalenga kuwakomesha watu kama
hao.
Mtandao huo umesema mbali na kuchukua hatua za kisheria pia
unalenga kutumia teknolojia mpya ya kubana uuzaji na utengezaji wa Likes
bandia.
No comments:
Post a Comment