Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa
jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia
ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka uliopita bila ya kukusudia.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa
kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu
saa mbili na nusu asubuhi na akasema
ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye
kesi hiyo.
Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo
cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani
kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili
wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia
apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
No comments:
Post a Comment