Kijana anayefahamika kwa jina la Saadam Hussein (14)
aliyeungua vibaya kutokana na hitilafu ya umeme.Akizungumza na gazeti hili
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi namba 23 iliyopo katika jengo la
Sewahaji, baba wa kijana huyo Hussein Ally alisema mtoto wake anayelala katika
chumba karibu na dukani, alisikia vitu vikidondoka, lakini alipojaribu kuamka,
akakutana na moto huo ukiwa umekolea.
Alisema kijana wake alitaka kuokoa mali zilizokuwa
zinateketea na moto, lakini moshi na ukali wa moto ulimzidi nguvu na kusabisha
kushindwa kuona na hivyo kuungua huku duka lote likiteketea.Alisema pamoja na
mali zote zilizokuwepo dukani kuteketea, lakini pia mauzo ya siku 9
yanayokadiriwa kufikia shilingi milioni 1.9 nayo yaliungua. “Kijana wangu
ameungua vibaya sana, hapa ninamuomba Mungu tu maana hata kuongea ni shida,”
alisema baba huyo kwa huzuni.Muuguzi aliyekuwa zamu, ambaye alikataa kutaja
jina lake kwa vile siyo msemaji wa hospitali hiyo, alisema kijana huyo ameungua
vibaya, ingawa bado hawajajua ni kwa asilimia ngapi
Saadam Hussein akiwa na Baba yake katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.“Kuna viwango cha kuungua, siwezi kujua ameungua kwa asilimia ngapi
lakini sehemu kubwa ya mwili wake
umeuungua vibaya,” alisema. Baba wa mtoto
huyo alisema kijana wake alikuwa akifanya biashara hiyo kwa lengo la kuanza
elimu ya sekondari ya binafsi na kutokana na kuungua kwa duka hilo, amebaki
hajui la kufanya, wkani hata gharama za matibabu hospitalini hapo zinamtesa.
Aliwaomba watu wote walioguswa na kuungua kwa mwanaye
kumsaidia kwa kutumia namba zake za simu ambazo ni 0786 89 51 14 au 0754 67 62
39.
Chanzo Gpl
No comments:
Post a Comment