Pages

Thursday, October 30, 2014

JAMBAZI SUGU LAKAMATWA NJOMBE LIKIWA NA BUNDUKI


Bunduki aina ya  Pump Action Shortgun iliyokamatwa Njombe.

Na James Festo, Njombe.

JESHI la Polisi Mkoani Njombe limethibitisha kuwa linamshikilia mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Elias Nguvumali (28) mkazi wa mtaa wa mjimwema mjini Makambako kwa kosa la kukamatwa na silaha  aina ya Pump Action Shortgun ikiwa na risasi tano.

Kwa Mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa iliyosainiwa na kamanda wa polisi mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani  ilisema kuwa tukio hilo lilitokea octoba 26 mwaka huu  majira ya saa 12:30 asubuhi ambapo mtuhumiwa alikutwa na silaha hiyo yenye namba za usajili 007700112 katika mtaa wa mjimwema.


Taarifa hiyo ilisema kuwa bunduki hiyo ilikuwa ndani ya mfuko na mtuhimiwa alikuwa akitumia silaha hiyo kwenye matukio ya uhalifu ambapo hubadilisha jina lake na kuitwa Nathan Nguvumali.

Katika hatua nyingine ilisema kuwa mshitakiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.

Wakati huo huo mtu mkazi mmoja wa Wilaya ya Makete Mkoani hapa Bi.Tumulikwe Sanga (49) amejeruhiwa baada gari ya jeshi walilokuwa wakisafilia kuacha njia na kugonga kalavati na kupinduka  katika kijiji cha Tandala

Taarifa hiyo ilisema kuwa tukio hilo lilihusisha gari lenye namba 5968 JWTZ aina ya Land Ashoke mali ya kikosi cha KJ(911 ambayo ilikuwa na watu 17 ambapo watano kati yao ni askari na 12 ni raia wa kawaida.

Gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari mwenye namba za usajili MT 84276 CPL Munishi Antony wa  KJ  911  Dodoma lilikuwa limetoka Dododma kuelekea Makete ambalo lilifeli bleki kwenye mteremko.

Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa wito kwa madereva kuwa makini pindi wanaendesha vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuvifanyia ukaguzi kabla na baada ya safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

No comments:

Post a Comment