Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia ramani ya Tanzania inayoonyesha mchoro wa reli ya Kati inayotarajiwa kujengwa upya na kwa viwango vya kisasa wakati alipokutana na uongozi wa juu wa makampuni ya China yakiongozwa na China Railway Group Ltd. Makampuni mengine ni SINOSURE, Exim Bank, China Development Bank na China Agriculture Development Bank. Rais Dkt. Kikwete yuko nchini China kwa ziara rasmi ya kikazi (State Visit).
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya China Railway Group Limited Bwana Li Changjin na msafara wake kuhusu mpango wa serikali ya Tanzania wa kujenga reli mpya na ya viwango vya kisasa kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma, Tabora kwenda Mwanza, Kaliua kwenda Mpanda hadi Ziwa Tanganyika. Mazungumzo hayo yalifanyika huko Beijing tarehe 24.10.2014.PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment