Pages

Tuesday, October 28, 2014

KAMANDA NZOWA ATUMIWA PAKA 3 OFISINI,JIONEE HAPA


Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa akiwa ofisini kwake.
MAAJABU! Paka watatu wenye macho mekundu walimshangaza Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa pale alipowakuta katika mlango wa ofisi yake na kumng’ang’ania miguuni.
Sakata hilo lilitokea wiki iliyopita wakati Kamanda Nzowa akitoka ofisini na mgeni wake aliwakuta paka hao mlangoni.Kufuatia hali hiyo, wageni na baadhi ya askari anaofanya nao kazi walionekana kushangazwa na tukio hilo huku wakijiuliza kwa nini paka hao wamzingire kamanda huyo na kuwaacha watu wengine?
Hata hivyo, baadhi ya wageni waliokwepo walihisi 



kuwa huenda paka hao walitumwa kishirikina na watu anaopambana nao kwa kuwakamata kutokana na kupatikana na madawa ya kulevya kwani ameweza kwa kiasi kikubwa kudhibiti biashara hiyo haramu hapa nchini.
Akizungumza na Uwazi, askari mmoja alisema Kamanda Nzowa amekuwa akipata vitisho na majaribu ya kila aina ikiwemo rushwa lakini kwa kuwa ni mcha Mungu mzuri anashinda.
Hadi wageni hao wanaondoka paka hao bado walikuwa wamemng’ang’ania kamanda huyo.
 Hata hivyo, kamanda huyo alirudi nyuma na kufunga mlango na kuwaacha paka hao wakiwa wamesimama nje ya mlango wa ofisi yake.

Mwandishi wetu alipomuuliza Nzowa kutokana na hali hiyo alisema ni mambo ya kawaida kwake na kinachomsaidia ni Mungu kwani kila mara amekuwa akisali.

No comments:

Post a Comment