Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya
kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu
dhidi ya binaadamu.
Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya
mahakama hiyo.
Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha
mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu.
Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za
kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.
Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la
kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi
mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.
Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali
ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo
kuendelea.
Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda, amewasili mahakamani
akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.
Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea
kwa niaba yake.
No comments:
Post a Comment