Landon Jones mwenye umri wa miaka 12 ni kijana aliyepoteza
hamu ya kula pamoja na ile ya kunywa kwa mwaka mmoja kufikia sasa nchini
Uingereza.
Mnamo mwezi Octoba mwaka uliopita kijana huyo aliamka akiwa
hana hamu ya kula wala kunywa.
Landon ambaye alikuwa kijana mwenye nguvu aliyependa
kukimbia,kupeleka baisklei pamoja na kucheza na marafiki zake.
Madaktari katika hospitali tano tofauti wameshindwa kubaini
ni nini kinachomsumbua kijana huyo.
Wazazi wake Michael na Debbie wametafuta tiba kwa udi na
uvumba lakini majaribio yote ya matibabu yameshindwa kufaulu.
Wataalam wanaamini kwamba Landon ni kijana aliye na ugonjwa
wa kipekee ulimwenguni.
Katika kipindi cha mwaka mmoja kijana huyo amepoteza kilo
nyingi za mwili wake .
Wazazi wake wamejaribu kila wawezalo kumshawishi mwana wao
kula ,lakini ni nadra kwa kijana huyo wa miaka 12 kutia chochote mdomoni.
Vile vile katika kipindi cha mwaka mmoja amekosa masomo kwa
takriban siku 65 mbali na kuwa wazazi wake wanasema kwamba hajakimbia kwa miezi
kadhaa sasa,huku akilazimika kuwaangalia rafikize kutoka dirisha la nyumbani.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment