Pages

Friday, October 24, 2014

KIJANA WA AUSTRALIA ALIYEJIUNGA NA IS ATOA ONYO KWA MAREKANI


Baadhi ya watu wanaounga mkono wapiganaji wa IS nchini Iraq na Syria.
Kijana raia wa Australia, Abdullah Elmir 'Abu Khaled' aliyejiunga na kundi la wapiganaji wa IS wanaopigana nchini Iraq na Syria ameonekana kwenye kanda ya video. 
Katika kanda hiyo kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 anawahutubia waziri mkuu wa Australia Tony Abbot pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama.

Kundi la wapiganaji wa IS wanaopigana nchini Iraq na Syria.Kijana huyo alisema "hatutasalimisha silaha zetu hadi tutakapofika katika ardhi yenu. '' 

Alitoroka kutoka nyumbani Australia mwezi Juni na kijana mwingine raia wa Australia na inaaminika alisafiri kwenda Syria kupitia Uturuki.


Msemaji wa serikali amesema kanda hiyo ni idhara ya tishop la kundi la Islam ic State kwa dunia nzima. 
''Na hiyo ndio maana Australia imejiunga na muungani wa wanjeshi wanaopigana dhidi ya ISIL nchini Iraq,'' alisema msemaji huyo. 

Katika kanda fupi ya video iliyowekwa kwenye mtandao, Abdullah Elmir waliwahutubia viongozi hao kwa kusema:''Kwa viongozi, kwa Obama,kwa Tony Abbott nasema hivi, hizi silaha tulizo nazo , wanjeshi hawa hatutakoma kupigana, hatutasalimisha silaha zetu hadi tutakapofika katika ardhi yenu. ''

"Hadi tutakapoweka bendera nyeusi katika kasri ya Buckingham Palace, una hadi tutakapoweka bendera yetu katika Ikulu ya Marekani, hatutasitisha vita,'' alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 17.

No comments:

Post a Comment