Kisa cha kushangaza kilitokea nchini Nigeria ambapo mwanamke
mmoja alipewa kichapo cha mbwa hadi akafariki kwa madai ya yeye kuwa mchawi.
Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege iliyokuwa inaruka
mtini kabla ya kugeuka na kuwa binadamu.
Umati wa watu ulikusanyika eneo alilokuwa mwanamke huyo
baahi wakinasa matukio kwenye simu zao za mkononi. Polisi wawili walilazimika
kurusha mabomu ya petroli kuwatawanya watu hao na kuwazuia kunasa picha za
mwanamke huyo
aliyekuwa anachapwa sana.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, mmoja alisema kuwa mwanamke
huyo dakika chache zilizopita alikuwa Ndege mtini kabla ya kugeuka na kuwa
mwanamke.
Ndege huyo alikuwa anazunguka mti mjini Oshodi , kisha
akagonga mlingoti wa stima kabla ya kuanguka ardhini ambapo aligeuka na kuwa
mwanamke.
Hii ni kwa mujibu wa wakazi wa mjini Oshodi wanaodai kuwa
mwanamke huyo alikuwa mchawi.
'Kitu cha kushangaza'
''Ni kitu cha kushangaza lakini ni cha kweli,'' alisema
bwana Sobowale.
"tulipozungumza na mwanamke huyo alidai kuwa na nguvu
za kiganga, na kwamba alikuwa amewaua watu kadhaa. Aliongeza kuwa alikuwa
anarejea kwa mumewe anayeishi katika eneo la Mushin kabla ya tyukio hilo.
Baadhi ya watu walianza kumpiga picha. ''
Video ya umati huo ukimtandika mwanamke huyo imeenea kama
moto msituni na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye mtandao wa kijamii wa
YouTube.
Mwanamke huyo alikuwa uchi wa mnyama huku ngozi yake ikiwa
inatoka baada ya kuchomwa.
Banke Idowu ni mmoja wa watu walionasa video ya mwanamke
huyo akiwa anachapwa na umati na kwamba alikuwa amearifiwa na wenzake kuhusu
mwanamke huyo alivyobadilika.
Aliambia BBC kuwa "sijawahi kuona jambo kama hili
maishani mwangu,lakini nimesikia na kuona tu kwenye filamu kwa hivyo
waliponiambia kuwa limetokea , mimi nimeamini. ''
Alisema angedhubutu kumuokoa mwanamke huyo umati huo
ungemgeukia na yeye.
Polisi hawajuzungumzia tukio hilo, hususan kabla ya umati
huo kukusanyika na kuanza kumchapa mwanamke huyo.
Alifariki mda mfupi baadaye huku mwili wake ukipelekwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu.
No comments:
Post a Comment