Katibu na Mwanasheria mkuu wa kampuni
ya ufuaji umeme ya IPTL, Bw. Joseph Makandege akiwaonyesha waandishi wa habari
(hawapo pichani) nakala ya hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya Tanzania
ikizuia benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Tanesco kuendelea
kuwabugudhi wamiliki wa IPTL na kuingilia uendeshaji wa mitambo yake. Kushoto
ni Meneja Rasilimali watu wa IPTL Bw. Aidan
Kaude.
·
Yasema Bw. Sethi kuendelea kusimamia mitambo ya
ufuaji umeme ya Tegeta.
Mahakama Kuu ya Tanzania imeiamuru
Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Shirika la Usambazaji Umeme
Tanzania (TANESCO) kuacha kuingilia utulivu,
umiliki,
usimamizi
na utawala wa Mitambo ya ufuaji umeme ya Bw. Harbinder Singh Sethi iliyopo Tegeta, na kusubiri
uamuzi wa
mwisho wa kesi
yao ya
msingi.
Kampuni ya Independent Power
Tanzania
Limited
(IPTL) na Pan
African Power
Solutions
Limited
(PAP)
zilifungua kesi kwa kuhoji uhalali
wa maamuzi
ya Kituo
cha Kimataifa cha Kutatua
Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) dhidi ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) na Martha Renju (anaedaiwa kuwa
msimamizi wa mali zake), ijulikanayo kama "Decision
on Jurisdiction and liability" iliyotolewa katika
kesi ya ICSD
namba ARB
/ 10/20.
Katika hukumu hiyo yenye kurasa 16 iliyoandikwa na Mhe. Dk. Fauz
Twaib
(Jaji)
na kusomwa kwa
niaba yake na Mhe.
Amri
Msumi
Hamisi
(Jaji),
mahakama kuu jana
iliwazuia
SCBHK
na / au
Tanesco
kuendelea
kuwabugudhi IPTL na
PAP -zinazomilikiwa na Bw. Sethi –
mpaka
pale uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya msingi itakapo amuliwa.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama mbele ya Bw.
Sethi (mmiliki
wa IPTL /
PAP)
na
Kieren
Day (Mkurugenzi
wa SCB-HK),
Mhe. Dk
Twaib
aliamuru
Tanesco
kutofanya biashara yoyote na SCB-HK
au Martha
Renju
kwa niaba ya IPTL /
PAP bila ya
idhini ya kimaandishi kutoka IPTL / PAP.
"Wadaiwa kwa
pamoja wanazuiliwa kufanya utekelezaji wa maamuzi iliyotolewa katika chombo cha kimataifa
ya ICSD
yenye namba ARB
/ 10/20
na kusambazwa kwa wahusika mnamo tarehe
12 mwezi Februari mwaka 2014, kwa
namna yoyote ile,
na kusubiri uamuzi wa
mwisho wa kesi yao ya mdai, " inasomeka sehemu ya hukumu hiyo.
Tanesco ambayo
iliwakilishwa na Wakili
wake Bw. Urassa,
pia imezuiwa kutolipa
kwa
SCB-HK
na
Martha
Renju
malipo yoyote
wanayostahili IPTL /
PAP bila
ya idhini ya
maandishi kutoka kwa IPTL /
PAP.
Mahakama pia imeizuia Tanesco kutotekeleza
au kukubaliana
na au
kuyatekeleza maamuzi ya ICSID, na kusubiri uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya msingi.
Jaji Mhe.
Dk
Twaib
alitupilia mbali hoja ya mwanasheria wa SCB-HK,
Bw.Charles
Morrison,
ambaye alisema kuwa mahakama
kuu ya Tanzania haipaswi
kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya ombi hilo sababu Tanzania ni mwanachama wa Kituo cha Kimataifa cha Kutatua Migogoro ya Uwekezaji
(ICSID)
ambayo pia inajulikana kama Washington Convention au ICSID
.
Kwa mujibu wa hakimu Dr. Twaib, Wakili
Morrison
alionya
kuwa kama Tanzania
aitotii wajibu
huo, itajiweka sehemu mbaya katika nyanja ya kimataifa.
"Kwa heshima
kubwa, nashindwa kuona mantiki ya utetezi wa Bw. Morrison na jinsi gani litaathiri mamlaka ya Mahakama
hii
la
kuikubali
ombi hili. Japokuwa Bw. Morrison amekwepa kusema moja kwa moja, maoni yake yamelenga kusema kwamba mahakama hii haina mamlaka ya kutoa amri husika.
"Ninashindwa kuelewa ni jinsi gani serikali ya
Tanzania, ambayo si
sehemu ya kesi
hii, itakuwa imevunja Mkataba wa Washington kwa sababu tu ya wananchi wake wawili ambao ni wafanyabishara binafsi,
wametafuta
amri
ya
kuzuia
utekelezaji
wa uamuzi
wa ICSID
kwa
misingi ya udanganyifu.
Sioni
ni jinsi
gani, kwa
kutumia mamlaka
yake katika
kutoa
maagizo
hayo, mahakama hii
itakuwa inaingilia majukumu ya kimataifa ya Tanzania chini ya Mkataba wa Washington," inasomeka
hukumu ya Jaji Twaib.
Sababu ya pili ya Bw. Morrison ya kuoma mahakama isikubali ombi hilo ilikuwa kwamba madai
hayo yanaweza kuwa yametolewa “miaka mingi iliyopita” wakati kesi ya ICSID ilipoanza na kubainisha kuwa hii ni kesi iliyokufa (tort case), ingekuwa imefanyiwa
kazi ndani ya
miaka
mitatu ya tarehe
ile.
Jaji Twaib
alitupilia mbali hoja
hiyo kwa
kusema, "Kwa heshima kuba kwa Bw. Morrison, hoja hii haina nguvu ya kisheria.
Kama
ilivyosemwa
na mwanasheria wa waombaji
(Bw.
Joseph
Makandege
na Bw.
Melkzedek
Lutema),
madai hayo yanatoa changamoto
kwa uamuzi wa ICSID
ambayo ulitolewa
mwezi Februari,
2014.
Madai, hayo baada ya kushindwa Aprili 2014, haiwezi ukasema imepitwa na wakati.
Nitaitupilia mbali pingamizi hilo.”
Kuhusu ombi kuwa shauri hilo lisikilizwe katika mahakama
ya Hong Kong na fedha zote zipelekwe hiko, wanasheria wote Bw. Makandege
na Bw.
Lutema
walisema
kuwa litakuwa sio kutenda haki kwa mteja wao, sababu kuna kiasi kikubwa cha fedha
kinahusika,
ambayo
itakuwa vigumu kuirejesha na kuwa itakuwa vigumu kwa IPTL/PAP kurejea katika hali yake
kwa
sababu SCB-HK
ni
ya nje na haina
mali
zozote kubwa
Tanzania.
Hii inampa Bw. Sethi
ushindi kwa mara nyingine miongoni mwa kesi kadhaa ambazo zimekuwa zikianzishwa na SCB-HK dhidi ya
IPTL/PAP.
No comments:
Post a Comment