Amri iliyowekwa na Chuo Kikuu cha Zimbabwe ya kuwazuia
wanafunzi kubusiana imeelezwa kuwa haina "mantiki", mwakilishi wa
wanafunzi ameiambia BBC.
Agizo kutoka mamlaka ya chuo kikuu imesema "ukikutwa
katika mkao wa kubusiana" katika kampasi ya Harare utaadhibiwa.
"Katika umri huu tuseme siruhusiwi kubusu au
kumkumbatia mtu... ni kukosa akili," Tsitsi Mazikana amesema.
Uongozi wa chuo kikuu haujasema lolote kuhusu
hatua ya
wanafuzni kupinga amri hiyo.
Amri hiyo ilitolewa mwanzoni mwa mwaka wa masomo kama sehemu
ya orodha ya vitendo vya utovu wa nidhamu ambavyo vinahitaji hatua za haraka
kuchukuliwa kutoka mabweni ya wanafunzi".
Sheria ya chuo kikuu cha Zimbabwe inaorodhesha mambo 11
ambayo ni "utovu wa nidhamu" ambayo yatawezesha mwanafunzi kufukuzwa
chuo.
Katika orodha hiyo ya mambo 11 pia inapiga marufuku
msongamano na kupika katika vyumba vya kulala.
Miongoni mwa amri za chuo kikuu cha Zimbabwe
Jambo la nne katika tabia ambalo litamlazimisha mwanafunzi
kufukuzwa linasema: "kukutwa katika mkao wenye kuonyesha kubusiana au
kufanya mapenzi hadharani".
Bi Mazikana, ambaye ni mwanafunzi mwakilishi wa jinsia,
amesema kuwa kampasi tayari ina sheria ngumu kwa wale ambao wanashirikiana na
jinsia nyingine.
Katika hosteli za mtu mmoja mmoja, kwa mfano, wakaazi wake
wanaruhusiwa kuwapokea wageni wao na kuishia sebuleni na wageni hawaruhusiwi
kufika katika hoteli hizo baada ya saa Nne usiku, amesema.
Bi Mazikana amesema amri hiyo haina chochote kuhusiana na
maadili na zaidi ya hapo ni kuwadhibiti tu wanafunzi ambao"hawafurahii
namna chuo kikuu hicho kinavyoendeshwa".
"kama walikuwa wakichukulia kila kitu kuwa ni cha
kimaadili wasingeweka kondom katika hosteli na katika zahanati, lakini...
kubusiana na kukumbatiana - hakuna kitu kisicho cha maadili hapo,"
ameiambia BBC.
Chama cha wanafunzi nchini Zimbabwe (Zinasu) amesema utawala
wa chuo kikuu umekuwa na tabia ya kuweka sheria zenye utata bila kushauriana na
vyombo vya wanafunzi.
Umoja wa wanafunzi wanaandaa pingamizi dhidi ya sheria
inayozuia kubusiana, kiongozi wa chama cha wanafunzi, Zinasu, Gift Maposa
amekiambia kipindi cha BBC cha Focus on Africa.
Tayari kumekuwa na sheria zinazoingilia haki za wanafunzi
kuandamana- iliyoanzishwa mwaka 1997 - ambayo imechochea hofu miongoni mwa
wanafunzi kufukuzwa.
Mwandishi wa BBC, Brian Hungwe kutoka mji mkuu, Harare,
anasema wanafunzidaima wanaushutumu utawala wa chuo kikuu kwa kujiweka mbali na
fikra za vijana.
Kinywaji cha bia kilipigwa marufuku katika kampasi miaka
saba iliyopita, sheria ambayo imepuuzwa kwa kiasi kikubwa.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment