Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, October 29, 2014

MAUAJI YA KUTISHA LUDEWA NJOMBE, ATANDIKWA NONDO KICHWANI HADI KUFARIKI

 Jeshi la polisi wilayani Ludewa likiondoka eneo la tukio


 majirani wakiuangaliwa mwili wa marehemu Mgimba.
Mtu mmoja  aliyefahamika kwa jina la Merkion Mgimba(Msuruisi) miaka 70 mkazi wa Ludewa Kijijini katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ameuawa kwa kupigwa nondo kichwani usiku wa kuamkia tarehe 28 oktoba 2014 akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Akitoa taarifa katika eneo la tukio mke wa marehemu Bi.Theodora Luoga alisema kuwa marehemu alitoka ndani majira ya saa 5 usiku kwa lengo la kujisaidia haja ndogo lakini ghafla alikutana na mtu nje ya nyumba yake na kuanza kupambana naye ndipo alipozidiwa nguvu na kukimbilia ndani akipiga kelele.


Bi.Theodora alisema baada ya kusikia kelele hizo sebuleni alilazimika kutoka chumbani ili aende kutoa msaada kwa mume wake lakini alipofungua mlango wachumbani alikutana na nondo iliyompata mkononi ndipo alipofanya uamuzi wa kutokea dirishani ili aende kuomba msaada lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwani alishuhudia mtu aliyevalia shati jeupe akitokomea gizani.

Alisema baada ya muuaji huyo kukimbia alirudi kuona hali ya mumewe lakini alimkuta tayari ameshaaga Dunia,hapo akachukua uamuzi wa kwenda kuwaeleza majirani na kiongozi wa mtaa ili kumsaka muuaji huyo ambaye hakuweza kumfahamu zaidi ya kushuhudia shati lake jeupe.

“Nilisikia mumewangu akikimbia kutoka nje na baadae kelele sebuleni ndipo nilipotoka ili kutoa msaada lakini nilipofungua mlango wa chumbani muuaji huyo alinipiga na nondo mkononi ikanilazimu kufunga mlango na kurudi chumbani nikisikia mume wangu akilia kwa uchungu,nikaamua kupitia dirishani ili niombe msaada kwa majirani ndipo nilipomuona muuaji huyo akikimbia kichakani”,Alisema Bi.Theodora.

Alisema muuaji huyo hajachukua kitu chochote zaidi ya kufanya mauaji,pia alithibitisha kuwa hii ilikuwa ni awamu ya pili kwani kunakipindi marehemu aliwahi kupambana na mtu nje ya nyumba yake nyakati za usiku na kumshinda mtu huyo alibeba nondo kama ilivyokuwa leo ila hakutambulia.

Aidha kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea tukio hilo alisema mpaka sasa bado jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wake ili kumbaini muujia taarifa kamili zitatolewa  upelelezi ukikamilika.

NA HABARI LUDEWA BLOG.

No comments:

Post a Comment