Mkutano wa mwenyekiti wa baraza la
wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee
umeingia dosari baada ya vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chama cha
mapinduzi CCM kuingia na mabango yao katika mkutano uliokuwa ukifanyika
kijiji cha Kyamiorwa kata Kashalunga wilayani Muleba na kusababisha
vurugu.
Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema Halima Mdee amepokelewa
leo katika kijiji cha Kyamiyorwa na kufanya mkutano na wananchi katika
kijiji hicho ambapo vijana wanne wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chama cha
mapinduzi CCM walipoingia katika mkutano huo huku wakiwa wameshikilia
mabango yao na kusababisha vurugu katika mkutano huo, vurugu hiyo
zimetulizwa na jeshi la Polisi na mpaka sasa jeshi hilo linamshikilia kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Mansud Amri ambaye
ametajwa kuhusika katika kufanya vurugu hizo.
Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti wa bara la wanawake wachama
cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee amewataka vijana
kutotumiwa na wanasia wanao lenga kuvuruga amani ya nchi na badala yake
watulie ili kujenga taifa lenye amani na utulivu.
Nao baadhi ya wafuasi wa chama hicho akiwemo mbunge wa viti maalumu
Conchester Rwamlaza wamewataka wananchi kutoiunga mkono katiba mpya na
akaongeza kuwa wananchi wanatakiwa kushiriki katika uchaguzi wa serikali
za mitaa na kuhakikisha wanachagua viongozi bora ambao wataliongoza
taifa hili kwa umakini.
No comments:
Post a Comment