Mwanamume ambaye kazi yake ni ya upishi nchini Australia,
anadaiwa kumuua mpenzi wake na kumkatakata vipande na kupika baadhi ya sehemu
zake za mwili.
Aliyafanya unyama huo kabla ya yeye mwenyewe kujitoa uhai
wake.
Marcus Volke, mwenye umri wa miaka 28, alijikataa koo yake
huku akiwatoroka polisi waliokuwa
wamekuja kufanya uchunguzi baada ya majirani
zake kuripoti kuwepo harufu mbaya mfano wa nyama iliyooza iliyokuwa inatoka
nyumbani kwa mwanamume huyo.
Maafisa wa polisi walipata sehemu za mwili wa mwanamke huyo
zikitokota kwenye sufuria iliyokuwa imejazwa kemikali huku vipande vingine
vikiwa kwenye karatasi za plastiki za takataka nje ya nyumba katika mtaa wa
kifahari za Teneriffe.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Brisbane Courier
Mail. Mwanamke huyo raia wa Indonesia bado hatajambulishwa rasmi.
Wapenzi hao waliokuwa wanaishi pamoja walikutana wakiwa
wanafanya kazi kwa meli za kifahari na wote walikuwa wameajiriwa.
Wakazi wa mtaa huo waliambia vyombo vya habari kuwa harufu
mbaya ilikuwa inatoka katika myumba ya Volke na ikazidi kuwa mbaya siku
ziliposonga.
"nilipotoka nje harufu hiyo ilisababisha machozi kutoka
machoni na hata kunifanya kujihisi mgonjwa,'' alisema mkazi mmoja. ''Ungedhani
chakula cha Mbwa au nyama ilikuwa imeachwa nje kwa siku kadhaa.''
Polisi wangali wanafanya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment