Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 24, 2014

MSAADA WAKO UNAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYU

Mtoto  Zabibu Salum Abdalah
---------------
Na Steven Augustino wa demasho.com, Tunduru.
MZAZI wa mtoto wa miezi sita Zabibu Salum Abdalah ,ambaye kichwa chake kina kuwa kikubwa kila siku tangu azaliwe ameomba msaada wa fedha ili kufanikisha kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.
Mama mzazi wa Mtoto Bi. Zainabu Mustafa Rajab,alisema kuwa Binti yake huyo alizaliwa April 24 mwaka huu katika hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru,na kwambatatizo hilo la kuanza kukua kwa kichwa chake lilianza kujitokeza mwezi mmoja baadaye.


Alisem abaada ya tukio hilo,walianza kuhangaika kutafutamatibabu katika hospitali mbalimbali ,lakini hadi leo juhudi zao zimegongamwamba ,baada ya kuandikiwa barua ya Rufaa inayowata kakumpeleka kijana wao huyo katika Hospitali ya TaifaMuhimbili.
Alisema kutokana na wanafamilia hao kutokuwa na uwezo kifedha taarifa hiyo imewakatisha tamaa ya kuokoa maisha ya kijana wao huyo hali ambayo imewafanya kuwaangukia Watanzania wenzao,ili kuomba msaada huo utakao jumuisha nauli ya kutoka Wilayani Tunduru mkoani
Ruvuma kwenda Jijini Dar es Salaam, pamoja na gharama za matibabu.

Bi Zainabu aliendelea kufafanua kuwa baada ya kuandikiwa barua hiyo
,yeye na mzazi mwenzie , walienda katika ofisi ya MkuuwaWilaya , ilikuomba msaada la kini waliambulia kupewa barua ya utambulisho wa kuwaomba msaada wananchi mjini humo, 
 Lakini hadi sasa hakuna msaada wowote walioupata kupitia mfumo huo wa barua.

Alisema kwa mtu atakaye guswa na tukio hilo anaweza kutuma msaada
wake kwa kutumia Simu na mba 0685179479 ya animtandao wa Airtel money.


Akizungumzia tukio hilo ,Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya yaTunduru
Dr. Alex Kazula, pamoja na kuthibitisha kuwepo kwa tukio la mgonjwa huyo,
alisema kuwa Hospitali yake imechukuwa uamuziwa kumpatia Rufaa hiyo,
baada ya maafisa tabibu waliopo Hospitalini hapo kutokuwa na ujuzi wakutibu maradhi hayo.

No comments:

Post a Comment