Bwana mmoja nchini Ufaransa amemuoa mke wa zamani wa baba
yake (mama yake wa kambo) baada ya kushinda kesi iliyodumu kwa miezi kadhaa.
Harusi ya Eric Holder, 45, na aliyekuwa mama yake wa kambo
Elisabeth Lorentz, 48, ilifanyika katika kijiji cha Dabo, karibu na mji wa
Metz.
Imeripotiwa kuwa mume wa zamani wa bi harusi,
ambaye ni baba
wa Bwana Holder, alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
Sheria za Ufaransa zinapiga marufuku ndoa kati ya watoto wa
kambo na wazazi wa kambo, lakini mahakama ilitoa uamuzi wa ndoa hiyo kufanyika.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ilipinga uamuzi huo wa mahakama
katika eneo la Lorraine, lakini ikaamua kutokata rufaa.
Awali, wawili hao walipeleka malalamiko yao hadi katika
ofisi ya Rais Francois Hollande - lakini walipata barua kuthibitisha kuwa ndoa
za aina hiyo ni marufuku.
Baada ya uamuzi wa mahakama, bi harusi alisema:
"Hatimaye, ile siku kuu imewadia!"
"Kwa kweli nina imani kuwa habari yetu itasaidia
wapenzi wengine waliopo kwenye hali kama hii, kwa sababu najua wapo
kadhaa," ameliambia shirika la habari la AFP.
Bi harusi huyo ameongeza kusema kuwa mume wake wa zamani
amekuwa "akiwaunga mkono" katika mapambano ya kisheria.
No comments:
Post a Comment