Pages

Sunday, October 26, 2014

Mtoto ashukiwa kuwaambukiza wengi Mali



Shirika la afya duniani WHO linasema kwa msichana wa umri wa miaka miwili ambaye alithibitishwa kuwa mgonjwa wa kwanza wa ebola nchini Mali alisafiri kilomita kadha kwa basi nchini humo huku akionyesha dalili za kuugua ugonjwa huo.
 Zaidi ya watu 40 ambao walikaribiana naye wametengwa. Huenda msichana huyo alisafirishwa kwenda nchini Mali na nyanyake baada ya mazishi ya 
 
mamake nchini Guinea moja ya nchi ambazo zimeathirka pakubwa na ugonjwa wa ebola.
 Utawala nchini Mali sasa umethibitisha kuwa msichana huyo ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Mayes alikokuwa akipewa matibabu.

Mwandishi wa BBC anayehusika na masuala ya afya anasema kuwa huenda ikawa changamoto kubwa kuwapata watu wengine ambao walikaribiana na msichana huyo.

No comments:

Post a Comment