Mfanyikazi mwengine wa kituo cha afya aliyemtibu Thomas
Dancun kabla ya kifo chake katika jimbo la Texas nchini Marekani amepatikana na
virusi vya ugonjwa wa Ebola.
''Tulijua kuna uwezekano wa kisa cha pili kuripotiwa ,na
tumejitayarisha kwa uwezekano huo''alisema Daktari David Lakey ambaye ni
kamishna wa idara ya afya katika jimbo la Texas.
Marehemu Dancun ambaye aliambukizwa ugonjwa huo nchini
Liberia ,alifariki katika hospitali ya Dallas siku ya jumatano.
Hatahivyo jina la muhudumu huyo halikutajwa.
Bwana Duncan alipatikana na virusi vya ugonjwa huo katika
mji wa Dallas mnamo tarehe 30 mwezi Septemba ,siku kumi baada ya kuwasili
kutoka katika ndege ya Monrovia kuelekea Brussels.
Aliugua siku chache baada ya kuwasili nchini Marekani,na
kuelekea katika hospitali ya Texas mjini Dallas akiwa na homa kali.
Lakini licha ya kuwaeleza madaktari kwamba alisafiri kutoka
nchini Libya,aliagizwa kwenda nyumbani
baada ya kupewa dawa za maumivu.
Lakini Duncan baadaye aliwekwa katika karantini katika
hospitali hiyo ,na kufariki baadaye licha ya kupewa dawa za majaribio.
Haijulikani iwapo afisa huyo aliyepatikana na virusi vya
ugonjwa huo alikaribiana na Duncan au la baada ya kuonyesha dalili ama wakati
alipolazwa hospitalini.
Afisa huyo alipatikana na homa siku ya ijumaa kabla ya
kuwekwa katika karantini ili kufanyiwa ukaguzi.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment