Kamanda wa Polisi mkoani Iringa (RPC),Ramadhani Mungi
Na Friday Simbaya, Iringa
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari
Lugalo ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu
wasiofahamika kisha kupora pikipiki yake ambayo haijafahamika namba za usajili.
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa (RPC),Ramadhani Mungi
amewaambia waandishi wa habari ofisini
kwake leo kuwa Salehe Khamis (18)
aliuawa tarehe 06/10/2014 majira ya saa 6:15 usiku katika Kitongoji cha
Kikungwe Igumbilo, Kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa.(Martha Magessa)
RPC alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni pamoja na kuwania
mali, ambapo hata hivyo, watuhumiwa wanatafutwa na jeshi la polisi.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia
mmoja dereva wa lori aina ya Isuzu kwa kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu
huko katika Kijiji cha Itimbo Kata ya Ihimbo, Tarafa ya Kilolo mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alimtaja
marehemu kuwa ni Linus Mwirafi (45) mkazi Kijiji cha Itimbo kwa kudondokewa na
lori hiyo baada ya kupinduka.
Alisema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 244 CNK aina
ya Isuzu likiendeshwa na Yoktani Kikula (25) mkazi wa Ipogolo lilipunduka na
kumdondokea mtembea kwa miguu huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.
RPC alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe
05/10/2014 majira 06:00hrs katika kijiji cha Itimbo wilayani Kilolo, mkoani
Iringa, na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva
amekamatwa.
No comments:
Post a Comment