Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la
Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi. Jeshi la
polisi la nchi hiyo limesema.Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya
mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.
Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga
mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.
Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini
limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.
No comments:
Post a Comment