Mji wa bandari wa Barawe nchini Somalia ambao ulikuwa umetajwa kuwa
ngome ya mwisho ya kundi la Al shabaab umethibitiwa na vikosi vya
serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika.
Mji wa
Barawe ulio umbali wa kilomita 200 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa
Mogadishu umekuwa chini ya udhibiti wa wanagambo wa Al Shabaab kwa miaka
sita.
Muungano wa Afrika unasema kuwa wanamgambo wamekuwa
wakiutumia mji huo kama kituo cha kupanga mashambulizi dhidi ya mji mkuu
Mogadishu.
Wapiganaji wa Al-Shabaab walianza kuondoka katika mji huo siku chache zilizopita.
No comments:
Post a Comment