Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa
Athuman Livigha
Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa
UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu
jana.
Profesa Mukandala alisema Profesa Livigha alikutwa
na
masaibu hayo akiwa nyumbani kwake Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es
Salaam, usiku wa kuamkia jana na kwamba, mwili wake umechukuliwa na polisi kwa
uchunguzi zaidi.
“Ni kweli, na mimi hizo habari tumezipata na watu wote
wamekwenda nyumbani kwake. Mwili umechukuliwa na polisi, tunasubiri taarifa
kutoka polisi,” alisema Profesa Mukandala bila kufafanua zaidi.
Aliongeza: “Mimi nilikuwa mjini, wenzangu wamekwenda
nyumbani kwake Bunju. Tumesikitishwa sana kwa kupotelewa na mwalimu wetu
mwingine katika mazingira kama hayo.”
Profesa mwingine wa UDSM, Jwani Kwaikusa, aliuawa Julai, 2010
kwa kupigwa risasi na watu waliodaiwa kuwa ni majambazi.
No comments:
Post a Comment