Pages

Friday, October 31, 2014

RAIS SATA WA ZAMBIA KUZIKWA NOVEMBA 11, 2014 JIJINI LUSAKA

Serikali ya Zambia imetangaza kuwamazishi ya Rais Michael Chilufya Sata (pichani) yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 11 Novemba 2014, katika eneo la makaburi lililotengwa rasmi kwa ajili ya kuzikwa Marais  linaloitwa Embassy Park, Lusaka, Zambia.
Mwili wa Rais Sata unategemewa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka, siku ya Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014. Mara baada ya mwili kupokelewa utapelekwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mulungushi ambapo watu wote watapata fursa ya kuuaga. Dkt. Guy Scott, Makamu wa Rais ataweka shada la maua.


 Taratibu za kuaga mwili wa Rais Sata zitafanyika katika Ukumbi wa Mulungushi zitaanza rasmi siku ya Jumapili tarehe 2 hadi  Jumapili tarehe 9 Novemba 2014. Misa ya kuaga itafanyika siku ya Jumannne, tarehe 11 Novemba 2014 katika viwanja vya mashujaa, Lusaka.  na baada ya hapo mwili utapelekwa Embassy Park kwa mazishi.

              
                  MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI, AMINA

UBALOZI WA TANZANIA, LUSAKA 

No comments:

Post a Comment