Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 8 kufa
katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya
mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali
ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru
iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda
Arusha
mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo
ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita
magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili
zitawajia punde.
No comments:
Post a Comment