Serikali imeamua kuanzisha usajili mpya wa namba za pikipiki (aina zote za pikipiki zenye magurudumu mawili na zile za magurudumu matatu) ili kurahisisha usimamizi na utawala wa vyombo vya moto.Utaratibu mpya unaanza rasmi tarehe 1/10/2014, Mmiliki anapewa muda wa miezi sita kusajili chombo cha moto bila adhabu.
Utaratibu huu utahusu chombo cha moto chenye magurudumu mawili hadi matatu. Chombo cha moto kitakachotumika kwa ajili ya biashara kitapewa kibao cha rangi nyeupe na chombo kwa ajili ya shughuli binafsi kitapewa kibao cha namba ya njano.
Usajili huu utafanyika katika ofisi zote za TRA naMmiliki anatakiwa kwenda TRA na kadi halisi ya gari na Tshs.10, 000/- kwa ajili ya kadi mpya.
No comments:
Post a Comment