Na Felix Mwagara, Nachingwea
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Nachingwea, Mathias Chikawe ametangaza rasmi kuwa atagombea
tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu ujao
na kulitetea jimbo lake. Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza
na wananchi pamoja na viongozi wa CCM wa Wilaya na Kata ya
Mtua, wilayani Nachingwea katika sherehe ya kuwapokea viongozi
na wanachama wapya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) waliojiunga na CCM wilayani humo.
Waziri Chikawe alisema wananchi wake bado wanamuhitaji kwa
hiyo hawezi kuacha kugombea nafasi hiyo kwani wazee na wananchi
mbalimbali katika Kata zote alizokuwa akipita kufanya mazungumzo
nao wanamuomba agombee tena nafasi hiyo.
“Wakati nikiingia ubunge mwaka 2005 katika jimbo hili kulikuwa
hakuna lami na barabara nyingi za kwenda vijijini zilikuwa hazipitiki na
pia maji yalikuwa shida lakini sasa barabara za lami mjini Nachingwea
zimejengwa, maji yanapatikana tena yasio na chumvi, barabara vijijini
zinapitika kwa kuwa zimechongwa vizuri kwa kuwawezesha wakulima
kupitisha mazao yao,” alisema Chikawe huku akishangiliwa na mamia
ya wananchi waliofurika katika sherehe hiyo.
No comments:
Post a Comment