Pages

Wednesday, October 29, 2014

Zinedine Zidane afungiwa miezi mitatu kufundisha soka

Chama cha soka cha Hispania kimemfungia kwa miezi mitatu Zinedine Zidane kwa kufundisha soka bila kuwa na vyeti vya utaalamu vinavyoruhusu yeye kuwa kocha.
Kiungo huyo hatari wa zamani  wa Ufaransa alikuwa anaikochi timu ya akiba ya Real Madrid Castilla, mabingwa wa ulaya.
Msaidizi wa Zidane, Santiago Sanchez pia naye amepigwa likizo hiyo ya lazima ya miezi mitatu.


Timu ya Real imesema haikubaliano na maamuzi hayo na watakata rufaa.
Klabu hiyo imesema kwamba Zidane ameruhusiwa na Shirikisho la soka la Ufaransa kufanyakazi kama kocha mkuu wa Real Madrid Castilla kutokana mna mazingira yanayokabili klabu hiyo kwa sasa.

Real imesema kwa sababu hizo itaendelea kutumia vyanzo vyote vya kisheria kuhakikisha kwamba uamuzi huo unasitishwa.
Zidane aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya akiba hivi karibuni baada ya kufanyakazi chini ya  kocha Carlo Ancelotti msimu uliopita uliowezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa.
Kiungo huyo wa uFaransa ameiechezea real Madrid kwa misimu mitano baada ya kujiunga nayo akitokea Juventus mwaka 2001 kwa gharama ya paundi milioni 45.8. Kipindi hicho gharama hizo zilivunja rekodi ya dunia.
Zidane alifunga goli la ushindi wakati Real ilipoitandika Bayer Leverkusen na kutwaa ubingwa wa Ulaya 2002, na akawa mwanasoka wa mwaka kwa mara ya tatu mwaka 2003.Alishawahi kupata tuzo hiyo mwaka 1998 na 2000. 
Mwaka 2006 aliondolewa nje ya mashindano ya kombe la dunia baada ya kumtwanga kichwa mchezaji wa Italia Marco Materazzi  kifuani. 
Zidane alifanyakazi kama mshauri wa Rais wa Real, Florentino Perez kabla ya kuwa mkurugenzi a masuala ya kispoti katika klabu hiyo mwaka 2011. 

No comments:

Post a Comment