Wanawake 8 wamefariki na wengine 50 wanaugua baada ya
kufanyiwa upasuaji wa kuwafunga vizazi nchini India.
Wanawake hao walielezea kuhisi maumivu makali na homa punde
baada ya kupewa matibabu hayo ya upasuaji wa kuwafunga uzazi katika kliniki ya
kiserikali huko eneo la katikati mwa India Chhattisgarh.
30 miongoni mwa walio hospitali hapo wanasemekana kuwa
katika hali mahututi.
Idara ya Afya nchi humo imeamuru uchunguzi ufanyike mara
moja.
Zaidi ya wanawake 80 walishiriki katika upasuaji huo wa
kuwazuia kupata uja uzito Jumamosi katika hospitali hiyo ya kijijini Pendari
huko Chattisgarh.
Baadhi ya wanavijiji wanadai shughuli hizo za upasuaji
zilifanywa na daktari mmoja na msaidizi wake katika mda wa masaa 6 tu hivyo
wanahoji iwapo ziliendeshwa vyema.
Miili ya Waliofariki ingali inafanyiwa uchunguzi .
Wanaougua wanapewa matibabu katika hospitali tofauti katika
eneo hilo.
Waziri wa Afya katika jimbo hilo ameiambia BBC kuwa
wanafanya wawezalo kuokoa maisha ya wanaougua na wameunda jopo litakalochunguza
kilichosababisha hali hiyo isiyo ya kawaida.
Serikali ya India hufanya utaratibu wa mara kwa mara wa
kutoa kwa ujumla huduma kwa wanaohitaji operesheni hizo za kufunga kizazi kama
njia moja ya kujaribu kudhibiti ongezeko kubwa la idadi ya watu nchini humo.
No comments:
Post a Comment