Mkuu wa Kijiji cha Maeneo huru ya
uwekezaji katika Mji wa Chengmai aliyevaa shati jeupe Bwana
Yang Si Tao akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif aliyepo kushoto yake wakati
ujumbe wa Zanzibar ulipoangalia maeneo hayo ukiwa katika
ziara ya siku 10 Jimboni Hainan.
Kushoto ya Balozi ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi,
Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima
Kombo Haji,Balozi wa Tanzania Nchini China Bwana
Abdullrahman Shimbo na Mkewe Mama Mary Antoni Tairo.
Nyuma ya Bwana Yang Si Tao ni Waziri wa Habari Zanzibar Mh.
Said Ali Mbarouk, Katibu Mkuu Fedha Nd. Khamis Mussa,Mye wa
Manispaa ya Zanzibar Msitahiki Khatib Abdulrahman, Katibu
Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala wa Mikoa na Idara
Maalum Nd. Joseph Abdulla Meza, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalis Salum
Mohamed, Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban,
Mhudumu wa Balozi Seif Hassan Ali pamoja na Mkurugenzi
Manispaa Nd. Abeid Juma Ali.
Balozi Seif na ujumbe wake wakifuatana
na mwenyeji wao Mkuu wa Kijiji cha Uwekezaji wa Mji wa
Chengmai Bwana Yang Si Tao wakielekea ukumbi wa mkutano kwa
mazungumzo.
Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd.
Salum Nassor Khamis, Mkurugenzi Mambo ya Nje Zanzibar Balozi
Silima Kombo haji.
Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ule mwenjeji wa
Hainan ukiongozwa na Gavana wa Jimbo hilo Bwana Jian Dingzhi
ukiendelea na mazungumzo yao ya uhusiano hapo katika Hoteli
ya Le Meriden Mjini Haikou.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif akimkabidhi zawadi wa Kasha lililojaa vyakula vya
viungo { spices } Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian
Dingzhi mara baada ya kumaliza mkutano wao rasmi wa
ushirikiano.
Gavana wa Jimbo la Kisiwa cha Hainan
Bwana Jian Dingzhi akibadilishana mawazo na Mgeni wake
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya
kumaliza mazungumzo yao.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment